ANDY MURRAY

KUSHIRIKI OPEN SUD DE FRANCE

Bingwa - - HABARI - PARIS, Ufaransa

KINARA wa tenisi, Andy Murray, atashiriki michuano ya Open Sud de France ambayo itakafanyika Februari mwakani katika mji wa Montpellier nchini Ufaransa.

Mashindano hayo ya 250 yatafanyika kuanzia Februari 3 hadi 10 ikiwa ni wiki moja baada ya kumalizika ya Australian Open.

Mwingereza huyo namba moja wa zamani, alihitimisha msimu huu Septemba mwaka huu akiwa amecheza mashindano mara 12, baada ya Juni mwaka huu kufanyiwa upasuaji wa mkono kwa kile alichodai ni kwamba anataka kujiweka fiti kwa ajili ya msimu wa mwaka ujao.

Katika maandalizi yake hayo tayari Murray ameshatangaza kushiriki pia michuano ya Australian Open ambayo itafanyika mwakani na mingine ya Brisbane International ambayo itafanyika mapema mwezi huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.