Lakers yamnasa Tyson Chandler

Bingwa - - HABARI - NEW YORK, Marekani

TIMU ya mpira wa kikakpu ya Los Angeles Lakers, imetangaza kumsajili nyota wa mchezo huo, Tyson Chandler, ambaye alikuwa akiichezea Phoenix Suns.

Kwa mujibu wa mtandao wa ESPN, msimu huu Lakers watamlipa Chandler kitita cha dola milioni 2.11.

Taarifa hizo zilieleza kwamba, Chandler alimaliza mkataba wake na Phoenix Suns mwishoni mwa wiki iliyopita na hivyo amesajiliwa akiwa mchezaji huru.

"Baada ya kuangalia mechi zetu 10 za kwanza, tumebaini kuna maeneo ambayo yanatakiwa kuzibwa na hivyo tukashauriana na kocha wetu mkuu Luke Walton tuimarishe kwanza safu ya ulinzi na ushambuliaji,” alieleza Meneja Mkuu wa timu hiyo, Rob Pelinka, kupitia taarifa aliyoitoa katika tovuti ya timu hiyo.

"Na ndio maana tumemsajili Tyson Chandler, ili atuongezee nguvu,” aliongeza kiongozi huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.