Solari aweka ngumu kuzungumzia kibarua chake

Bingwa - - SPORTS - MADRID, Hispania

KOCHA wa muda wa timu ya Real Madrid, Santiago Solari, amekataa kuzungumza kuhusu hatima yake ya baadaye katika kikosi hicho akisema kwamba kwa sasa anachokiwaza ni kuhusu mechi zijazo zinazowakabili.

Tangu akabidhiwe mikoba hiyo, Solari, alishaiwezesha timu hiyo kushinda mechi tatu mfululizo ukiwamo wa juzi ambao waliiadhibu Viktoria Plzen kwa mabao 5-0 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Ninachokiwaza pekee ni kuhusu mechi ijayo. Na kama nilivyowahi kusema tangu mwanzo nitajaribu kuirejesha timu kwenye mstari, sidhani kama hilo litakuwa baya,” alisema kocha huyo.

"Soka mara zote ni mchezo wa ajabu hivyo jambo la muhimu ni kuwazia mechi inayokuja siku moja kabla na ni kama hii, wachezaji walikuwa vizuri kwa hiyo kuanzia sasa tunawazia inayokuja,” aliongeza kocha huyo.

Mechi ijayo ya Real Madrid itakuwa ni Jumapili wakati ikapokuwa ugenini ikiikabili Celta Vigo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.