Stars yatua ‘Sauzi’ na kuanza kujifua

Bingwa - - MAONI MTAZAMO KATUNI - NA MWAMVITA MTANDA

BAADA ya kutua nchini Afrika Kusini juzi, wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, hawakuwa na muda wa kupumzika bali kuendelea na mazoezi ya nguvu kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho.

Katika kujiandaa na mtanange huo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani, Stars itafanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Celtic Bloemfontein nchini humo.

Akizungumza na BINGWA kwa njia ya mtandao jana, kocha mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Amunike, alisema baada ya kufika hakutaka kuwapumzisha wachezaji na badala yake alianza kuwapa programu ya mazoezi.

“Hatukuwa na muda wa kupoteza hasa ukizingatia zimebaki siku chache kabla ya mchezo, lazima niwaandae wachezaji vizuri maana hatujui wenzetu wamejipanga vipi,” alisema Amunike.

Aidha, alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba kikosini hakuna majeruhi na wachezaji wote wamekamilika, hivyo kikubwa ni kupambana kuhakikisha wanarudi na ushindi nyumbani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.