Ukata wakwamisha kambi soka la ufukweni

Bingwa - - MAONI MTAZAMO KATUNI - NA MWAMVITA MTANDA

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni, Boniface Pawasa, amesema kwamba, hali ya ukata inayowakabili inawakwamisha kuingia kambini mapema.

Kikosi hicho kinakabiliwa na kibarua kizito katika michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, inayotarajiwa kuanza Desemba 8 hadi 14, mwaka huu nchini Misri.

Akizungumza na BINGWA jana, Pawasa, alisema mwingiliano wa ratiba za mechi mbalimbali za kimataifa zinazotarajiwa kuchezwa hivi karibuni ikiwano ile ya Taifa Stars dhidi ya Lesotho, umechangia kuwepo na uhaba wa fedha unaowafanya washindwe kuanza kambi kwa wakati.

Aidha, Pawasa aliwaomba wadau, mashabiki na kampuni mbalimbali kujitokeza kuichangia timu hiyo ili ifanikishe malengo yao ya kambi.

“Timu ni ya Watanzania hivyo lazima tusaidiane kuhakikisha mambo yanakwenda sawa, naomba wadau wajitokeze kutusaidia,” alisema Pawasa.

Kikosi hicho kinaendelea na mazoezi kila siku asubuhi katika fukwe za Coco kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya Afrika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.