Nadal kuzikosa mechi za mwezi huu

Bingwa - - HABARI - LONDON, England

STAA wa mchezo wa tenisi, Rafael Nadal, atalazimika kuikosa michuano yote ya mwezi huu ya fainali za Chama cha Tenisi Kimataifa, ATP, zitakazofanyika jijini London, baada ya kufanyiwa upasuaji wa enka.

Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni baada ya Nadal mwezi uliopita kujitoa katika michuano ya Paris Masters, kutokana na matatizo ya misuli ya nyama za paja jambo ambalo lilimfanya Novak Djokovic, amwengue kwenye nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora duniani.

Akizungumza juzi Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 32, alisema kuwa wakati akiwa bado anauguza matatizo hayo, ni bora pia akaitumia nafasi hiyo kufanyiwa upasuaji huo wa enka.

"Kwa bahati mbaya wiki iliyopita nikiwa mjini Paris nilipata matatizo na wakati huo nikakumbwa na matatizo ya enka ambayo yanatakiwa nifanyiwe upasuaji,” alisema staa huyo.

"Ukweli ni kwamba yamekuwa yakinisumbua kwa muda mrefu kitu ambacho nimekuwa nikikichukia,” aliongeza staa huyo.

Alisema hata hivyo ana uhakika wa kuwa fiti kuanzia msimu ujao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.