Stand United yawapotezea wakongwe

Bingwa - - KOLAMU/HABARI - NA TIMA SIKILO

KOCHA msaidizi wa Stand United, Athumani Bilali ‘Bilo’, amesema hawana mpango wa kutoa au kusajili mchezaji kutoka timu za nje katika dirisha dogo la usajiri badala yake watapandisha wale wenye uwezo wa kikosi chao cha vijana.

Akizungumza na BINGWA jana, Bilo alisema wachezaji wengi wa mkopo wanakuwa hawajatumika kwa muda mrefu katika vikosi vyao, hivyo kuwasajili ni kama kuongeza tatizo ndani ya kikosi chao.

Alisema timu yao ya vijana ina wachezaji wazuri sana ambao kila siku wanatumika hivyo wao wataboresha kikosi chao kwa kuwapandisha baadhi yao. “Tunawaamini wachezaji wetu, tumewalea wenyewe na mashabiki wasiwe na wasiwasi watacheza mpira mzuri, timu itakuwa pazuri watafurahi,” alisema.

Stand United leo wanatarajia kuvaana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wao wa 15.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.