Gadiel: Nipo fiti kurejea mzigoni

Bingwa - - KOLAMU/HABARI - NA TIMA SIKILO

BEKI wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael, amewapa moyo mashabiki wa timu hiyo kuwa anaendelea vizuri na kwamba atajiunga na wenzake watakaporejea Dar es Salaam wakitokea Mbeya.

Yanga wanaoongoza Ligi Kuu Tanzania Bara jana walitarajiwa kuvaana na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine.

Gadiel alipata majeraha katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui uliochezwa Novemba 22, mwaka huu mkoani Shinyanga na kutakiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki moja.

Akizungumza na BINGWA jana, beki huyo anayechezea pia timu ya Taifa, Taifa Stars, alisema muda ambao madaktari walimshauri kukaa nje ya kikosi umeisha, hivyo yupo tayari kuanza cheche zake.

“Kukosekana kwenye kikosi changu kunaniumiza, lakini siwezi kulalamika kwa sababu ninaumwa na ili nicheze vizuri lazima nijiuguze,” alisema Gadiel.

Gadiel ni miongoni mwa mabeki wa Yanga ambao wanapewa nafasi kubwa ya kucheza na kocha wao, Mwinyi Zahera.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.