CHERYL APEWA MCHUMBA NA MASHABIKI

Bingwa - - MAKALA -

LICHA ya kwamba hawana uhakika wowote, mashabiki wa mwanamuziki Cheryl, wanahisi bibiye huyo anatoka kimapenzi na mwigizaji wa Hollywood, Michael B Jordan.

Hiyo ni baada ya Cheryl (35) kuwa sambamba na jamaa huyo katika mahojiano yake na kipindi cha runinga cha Graham Norton mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika mahojiano hayo, Cheryl anayetamba na wimbo wake ‘Love Made Me Do It’, alionekana akijishaua mbele ya Michael mwenye umri wa miaka 31, hivyo mashabiki kuamini kuwa wanatoka kimapenzi.

“Michael B Jordan atakuwa mchumba wa saba wa Cheryl,” aliandika shabiki mmoja katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

Kwa kipindi kifupi cha miaka miwili iliyopita, Cheryl ameshuhudia ndoa zake mbili zikivunjika, ya kwanza ikiwa ni ile aliyofunga na beki wa zamani wa Chelsea, Ashley Cole.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.