Drake ambwaga dada aliyedai kubakwa

Bingwa - - MAKALA -

RAPA Drake ameshinda kesi ya ubakaji aliyokuwa amefunguliwa na mwanamke mmoja, taarifa hiyo imeripotiwa na mtandao maarufu wa habari za mastaa, TMZ.

Kwa mujibu wa TMZ, Drake, mwanamke huyo anayeitwa Layla Lace, alifikisha madai yake mahakamani Aprili, mwaka jana na si kubakwa tu, pia alisema amepewa ujauzito.

Aidha, baada ya uchunguzi wa mahakama, imebainika kuwa bibiye Layla alidanganya lakini hajatupwa gerezani, bali amepewa onyo kali akitakiwa kutorudia.

Mwanasheria wa Drake, Larry Stein, amesema wameridhishwa na hukumu hiyo na Drake amewashukuru wote waliokuwa wakimuunga mkono katika kesi hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.