ULEVI WAMPONZA MCHEKESHAJI, AANGUKA CHALI JUKWAANI

Bingwa - - MAKALA - LOS ANGELES, Marekani

JUMAMOSI ya wiki iliyopita ilikuwa siku mbaya kwa mchekeshaji, Johnny Vegas na huenda kilichomkuta kikabaki kwenye kumbukumbu zake.

Akiwa jukwaani, staa huyo wa kuvunja mbavu alianguka ghafla na ndipo mashabiki wake waliposema hali hiyo ilitokana na kiasi kikubwa cha pombe alichokuwa amejitwisha kichwani.

Mashabiki waliohudhuria ‘shoo’ yake katika Ukumbi wa Philharmonic ulioko jijini Liverpool, walisema mshikaji alikuwa ameuchapa kinoma na waliligundua hilo kwa kuwa hata jukwaani hakuwa akizungumza vizuri. Video iliyosambaa mitandaoni inamwonesha Vegas (48) akisaidiwa kutembea na watu wake, jambo ambalo limewafanya mashabiki wake kusema wamechoshwa na tabia yake hiyo ya ulevi. Kwa upande wake, akitumia ukurasa wa Twitter, mmoja kati ya mashabiki wa kike alisikika akisema tungi hilo lilitokana na mkwanja mrefu aliouvuna kutokana na malipo mazuri ya onesho hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.