Klopp aomba radhi kwa kutimua mbio uwanjani

Bingwa - - MAKALA -

KOCHA Jurgen Klopp, amesema kwamba ameshamwomba radhi mwenzake wa Everton, Marco Silva, kwa kitendo chake cha kutimua mbio na kuingia uwanjani wakati akishangilia bao lililofungwa dakika za mwisho na nyota wake, Divock Origi na kuwapa ushindi katika mtanange huo wa Merseyside ‘Derby’.

Mechi hiyo ya juzi kati ya Liverpool na Everton ilionekana kama ingemalizika kwa matokeo ya sare tasa, kabla ya mlinda mlango, Jordan Pickford, kufanya makosa yaliyomwezesha Origi kuipatia timu yake bao hilo dakika ya 96 wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Anfield.

Bao hilo ndilo lililomnyanyua Klopp na kwenda kumkumbatia mlinda mlango wake Alisson wakati timu yake ikishangilia bao hilo la Origi upande mwingine.

Hata hivyo, kocha huyo wa Liverpool alikiri kupitiwa katika mahojiano na BBC Sport mara baada ya mechi hiyo.

"Awali ya yote ningependa kuomba radhi kwa kukimbilia uwanjani," alisema Klopp. "Kwa haraka nilishamwomba radhi Marco Silva, sipendi kuwa mtu asiyejiheshimu. Heshima yangu kwa Everton haiwezi kuwa kubwa baada ya mechi hii. Tunafahamu jinsi walivyo vizuri, lakini leo walikuwa vizuri zaidi na wagumu jinsi walivyokuwa wanacheza,” alisema kocha huyo.

"Bao lilikuwa ni bahati, lakini mawazo yetu yalikuwa wazi kwani tulipanga kusaka ushindi hadi dakika ya mwisho. Tulitaka kuonesha jinsi ya kuwatumia mastraika, ilikuwa ni mechi ndefu na ya wazi,” aliongeza kocha huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.