Mashabiki wamtegua kocha mkono

Bingwa - - JUMANN | UNAKOSAJE? -

KOCHA wa timu ya Mwembeni, Michael Emmanuel, aliteguka mkono baada ya mashabiki kumbeba juu wakati wakishangilia timu hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mbao 4-1 dhidi ya Makuti FC, katika mchezo wa Kombe la Kuku, uliochezwa kwenye Uwanja wa Manzese, jijini Dar es Salaam. Baada ya dakika 90 kumalizika, mashabiki walimwinua juu na kuanza kumrusha rusha huku wakimpongeza kwa kikosi kizuri lakini dakika mbili mbele walimwachia na kuanguka chini na kuteguka mkono wake wa kushoto.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.