Shabiki aponzwa na Arsenal, atoa 25,000/-

Bingwa - - JUMANNE SPESHO | UNAKOSAJE? -

SHABIKI wa Manchester United, Filipo John, alijikuta akitoa Sh 25,000 na kumkabidhi shabiki wa Arsenal, Mohammed Shukuru, baada ya kudai kuwa timu hiyo haiwezi kushinda katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham, uliochezwa juzi. Shabiki huyo wa United alisema Arsenal imezoea kufungwa hivyo endapo ingeshinda angetoa kiasi hicho cha fedha na kumkabidhi mwenzake huyo ambapo alitekeleza ahadi yake hiyo baada ya mchezo huo kumalizika na Arsenal kushinda mabao 4-2.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.