TOREIRA AFICHUA KILICHOWAUA SPURS

Bingwa - - MBELE -

KIUNGO wa Arsenal, Lucas Torreira, amesema maneno waliyopewa na kocha wao wakati wa mapumziko ndiyo yaliyowapa ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya mahasimu wao wa Kaskazini mwa Jiji la London, Tottenham.

Arsenal walikwenda mapumziko wakiwa wameshapachikwa mabao 2-1, lakini waliweza kufufuka kipindi cha pili na kuibuka kidedea katika mtanange huo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa katika Uwanja wa Emirates.

"…Tulimsikiliza kocha na tukaimarika kwa kiasi kikubwa. Hiyo ndiyo iliyokuwa siri ya ushindi," alisema Torreira ambaye ndiye aliyetajwa kuwa nyota wa mchezo.

Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa raia huyo wa Uruguay kupewa heshima hiyo katika michezo minne iliyopita na bao lake dhidi ya Tottenham lilikuwa la kwanza tangu kutua Arsenal.

Matokeo hayo yamefanya Gunners kusogea hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kama wataifunga Manchester United usiku wa kesho, basi itakuwa ni mechi yao ya 19 mfululizo bila kufungwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.