Ibrahim Pasha anashinda kesi dhidi yake, Hadija na dada yake wanatofautiana

Bingwa - - MBELE - MAONI NA USHAURI 0755625042

KATIKA mwendelezo wa simulizi yetu leo tuanze moja kwa moja kwa ndugu wawili Mehmet na Mihrimah wakibishana kuhusu ujauzito aliobeba mmoja wa masuria wa harem lao.

Mihirimah anamtaka Mehemet abadilike anaonekana ametoka kwa Nurbahar, Mehemet anauliza kama amekuwa kimapenzi na Taslicali kwa muda mrefu lakini Mihrimah anajibu hakuna na wala hakitakuja kutokea kitu kama hicho.

Sasa mbona unaniogofya, ukimnya wako utalipwa kwa ukimya wangu, anasema Mahmet akimweleza Mihrimar kwamba hataki Taslicali ateseke kwa sababu tu eti amezungumza naye, hawamruhusu kueleza, kujiimarisha kwamba si mkosefu naona wanaweza kumpoteza.

Mehemet anamwambia Mihrimah amweleze ukweli anamwambia huo ndiyo ukweli, ameitwa na Ibrahim Pasha ndiyo tukaonana, Mihrimar anamweleza kaka yake kwamba anachoona ni bora azingatie haki zake na mambo yake.

Anamweleza akishindwa kufanya anayomshauri na baba yake akajua hatakwenda jimboni kwake kamwe, Mehemet anauliza kama kuna njia nyingine tofauti na kutoa mimba anaelezwa hakuna.

Fidarh anafika anamuulizia Mahdervan anaulizwa kwanini anapaniki kuna nini kimetokea. Naelezwa ni ujumbe muhimu wanakwenda.

Ujumbe umekuja kwa daktari ukieleza kwamba Ayse Hatum msichana aliyewahi kulala na Mustafa ni mjamzito wa miezi miwili sasa.

Mahdervan anamfuata anamweleza Mustafa kwamba anatarajia kupata mtoto mwingine, baada ya kupitia kipindi kigumu wanakumbatiana kwa furaha.

Jaji Mkuu Kadi Efendi anawaita Ibrahim mtoto wa Abdullah na mshitakiwa Seyfi Bayrama, badala ya Ibrahim kusimama mbele ya jaji mkuu anasimama Naseuh Efendi anaeleza namna walivyokwenda msikitini na Ibrahim usiku huo.

Baada ya swala kuna watu walikusanyika nje na kumdhihaki Waziri Mkuu wetu Ibrahim. Jaji anauliza je, Seyfi Effendi alikuwa mmoja wao, anajibu ndiyo lakini hayo yakiendelea pia Sultan yupo anasikiliza mwenendo wote wa kesi hiyo unavyoendeshwa.

Maneno gani yameelekezwa kwa Pasha anauliza Jaji Mkuu, anajibiwa wamesema Ibrahim ni kafiri, mpagani, mkristu anayejificha anayevaa msalaba kifuani kwake na anakwenda kanisani vitu vingi wamemtuhumu.

Wakati kesi yake ikiendelea, Ibrahim Pasha anaendelea kukutana na mabalozi wa Ufaransa, anawauliza anavyoendelea mfalme wao anajibiwa kuwa yupo poa anasubiri maneno yake mazuri ya ushirikiano.

Pasha anatazamana na Ayas Pasha, anawauliza kwani bado mnaendeleza mahojiano na sisi, lakini msijali tutafikia makubaliano. Wajumbe hao wanashukuru kwa hilo huku wakimpa pole Ibrahim kwa kesi inayomkabili.

Anawajibu kwa ubabe kwamba taifa la Ottoman si taifa la kikabila linaongozwa na sheria na kupitia sheraia hizo ndizo zinazoamua. Kesi inaendelea Jaji Kadi Efendi anamuuliza Seyfi Effendi ajieleze naye kama Nasuh Efendi anasema ukweli, anajibu ni kweli amesema ukweli.

Seyfi anasema lakini kila kitu kinajidhihirisha maana hata kwake amejitengenezea masanamu ni sehemu ya kanisa lake na watu wanasema huwa anabadilishana nao baadhi ya vitu vya thamani ya dhahabu na wageni kutoka nje.

Jaji anamweleza umeongeza ya kwako nilichotaka ni kufahamu kama alichoongea Nasuh Efendi ni sahihi ama la, anajibu kuwa anaapa kila mtu amesema na anatamani naye ajionee kwa macho yake, jaji anamuuliza unaweza kuthibitisha tuhuma hizo anajibu hapana.

Lakini anafahamu kuwa amejiwekea sanamu, sawa umeshuhudia Pasha akipiga hilo jiwe, anajibu hapana sijaliona, au ulisikia watu wakiongea anajibu alisikia wakiongea.

Jaji Efendi anamtaka aeleze kwanini aliamini upumbavu wa kutokuona wala kusikia anampa mifano ya kwenye vitabu vitakatifu, anayemtuhumu mtu au kuzungumzia ya mtu yeye mwenyewe anakuwa haaminiki.

Anajitahidi kujitetea kwamba dalili za moto ni moshi lakini Jaji anasimama katika misingi ya sheria anamweleza umemkosea Ibrahim Pasha unastahili adhabu yeye anajibu kwamba hayo si mashitaka yake, amesema machache tu, anapewa nafasi ya kueleza hayo yake lakini anasema amesahau.

Jaji Efendi anasema itakuwa kuna mtu amesema maneno hayo naye ukayafuata kama alivyosema neno kwa neno ndiyo maana umesahau.

Shah anamuuliza Hadija taarifa zozote kuhusiana na kesi ya Ibrahim Pasha anamweleza hajapata taarifa zozote, Shah anamjibu Ibrahim anastahili mapenzi yake, Hadija anashangaa kwanini amesema hivyo anamuuliza kwanini umesema hivyo, anajibiwa kwanini alimficha alipogundua kuwa alikuwa na uhusiano na Nigar Khalfa na akapata mtoto naye.

Hadija anamweleza dada yake kwamba anajua Hurrem ndiye amemweleza hayo, Shah anajibu ndiyo na inawezekana hana hata hatia kwa hayo unayomtuhumu nayo tatizo lipo kwako na Ibrahim wako.

Nafahamu upo

Jaji anamjibu kama angekuwa na kazi asingekwenda mahakamani angeendelea na kazi zake, anajitetea tena akimtaka Kadi Efendi basi yaishe, yaishe.

upande wake tangu ulipofika hapa ameshakujaza sumu zake, Shah anajibu asifananishwe na yeye hawezi kumtokea mambo kama hayo na haitaweza kutokea.

Kesi ya Ibrahim Pasha inaendelea baada ya kusahau maneno anaieleza mahakama kwama Ibrahim Pasha alimwambia amkate kichwa lakini anaamini hana nguvu hiyo, ni kosa kuwa, anasema yeye ni mfanyabiashara anayeaminika mno hivyo anamuomba Jaji amruhusu akaendelee na majukumu ya kazi zake.

Jaji anamjibu kama angekuwa na kazi asingekwenda mahakamani angeendelea na kazi zake, anajitetea tena akimtaka Kadi Efendi basi yaishe, yaishe.

Jaji anamwambie anyamaze anamuuliza Nasuh Efendii kama ana la nyongeza kuhusiana na kesi hiyo, anajibu hana la kuongeza.

Jaji anaeleza kwamba Ibrahim Pasha anayo mamlaka ya kufanya alichokifanya ingawa hakuna mtu anayefikiri yupo juu ya sheria na sitaruhusu mtu yeyote avunje ama kuharibu sheria bila maamuzi ya mahakama.

Anaandika hitimisho la kesi hiyo kwamba Seyfi Effendi amekiri kutenda kosa la kumdhihaki Ibrahim Pasha kwa kosa hilo atapata adhabu kali ya viboko 100 makalioni na atafungwa

miaka kumtaka jaji amuokoe na adhabu hiyo nina watoto waangalie wataishije nikiwa kifungoni.

Jaji anajibu kuwa alitakiwa kufikiria kabla ya kutenda aliyotenda. Na nimarufuku kwa yeyote kusema uongo chochote utakachosema mbele ya mahakama utatakiwa kuthibitisha, kesi imeisha mpelekeni akaanze kutumikia adhabu yake Seyfi analalamika huku akiomba huruma ya Jaji Kadi Efendi.

Lakini Kadi Efendi anapoangalia pembeni macho yake yanakutana na macho ya Sultan akiwa amejifunika ili asijulikane, Sultan anampa ishara Kadi Efendi kwa kutingisha kichwa chake naye anafanya hivyo.

Ibrahim Pasha naye na wageni wake anawaeleza kuwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu hapo umekuwa mwisho mengine atawatumia kwa maandishi wanakubali lakini baada ya hapo wanamweleza Ibrahim kwamba kitabu alichoomba kitaletwa kwake na meli zinazotarajiwa kutia nanga siku chache zijazo, lakini Pasha anawaeleza alitaka kusoma kitabu hicho muda mrefu na si sasa.

Wakiwa katika mazungumzo hayo, Nasuh Efendi anafika kuonana na Ibrahim Pasha wananong’onezana wanaelewana, anamweleza mjumbe huyo kutoka Ufaransa kwama kama anataka kufahamu maamuzi ya mahakama afuatane naye sokoni atafahamu yeyote anayefanya jambo kwa kumpinga nini kinamtokea.

Baada ya kesi hiyo, Sultan anamfuata kwa mazungumzo anamweleza ilikuwa kesi yenye msimsimko mno na ugumu kwake lakini kwa mara nyingine kwamba haufanyi maamuzi kwa utashi wako wala kuegemea upande wowote unachofuata ni sheria tu.

Sultan anamweleza kwamba anafikiri kipindi cha mfungo wa Ramadhani hatapata shida lakini Jaji anajibu alipata tabu alipokwenda kukagua sokoni akakuta biashara ya nyama imekuwa na changamoto kubwa lakini hakutueleza kwa wakati.

Sultan anajibu kwanini Kadi Efendi hukuchukua namna nyingine ili nyama ipatikane maana jiji lote la Instanbul ni lako unawajibika wewe.

Aliyekuwa na jukumu la kuagiza nyama ahakuagiza kwa sababu zake binafsi lakini nimechukua hatua nyingine nyama itakuja kutoka nchi jirani, yule aliyekuwa akileta kwetu ameiuza Poland.

Sultan anataka aandikiwe maelezo yote kuhusu kukosekana nyama na namna alivyofanya njia mbadala wa kupatikana kwa nyama hiyo.

Sumbula anamletea taarifa Hurrem kwamba Ibrahim Pasha ameshinda kesi Hurrem anachukia anaelezwa hadi Sultan alikuwepo kwenye kesi anataka aitiwe Ayas

Pasha. Wakati hayo yakiendelea, Ibrahim Pasha anafika sokoni ambapo aliyekutwa na hatia anapata adhabu ya viboko adharani, Rostima anashuhudia. Hadi kesho katika mwendelezo wa simulizi hii usikose kufuatailia hapa hapa, maoni, ushauri 0755625042. Usibipu tafadhali.

mitano huko visiwa vya Rhodes, Seyfi anatoa sauti ya

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.