Mshindi bajaj SportsPesa afunguka furaha yake

Bingwa - - KOLAMU/HABARI - NA MWANDISHI WETU

MSHINDI wa droo ya 63 promosheni Shinda Zaidi na SportsPesa, Malick Rashid, amesema anaamini maisha yake yataboreka kiuchumi na kuongeza mtaji kwenye biashara ya uwakala anayofanya ya mitandao ya simu.

Rashid mwenye umri wa miaka 19 alikabidhiwa bajaj yake na timu ya Shinda Zaidi na SportPesa iliyomtembelea Mtamba mkoani Morogoro.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa bajaj, Rashid alisema wakati anapigiwa simu na SportPesa hakuamini kwa muda ule kama ni kweli ameshinda.

Alisema alitulia na kufuatilia zaidi na baada ya muda akapigiwa tena simu na kupewa maelekezo namna ambavyo bajaj itamfikia na hapo ndipo ilikuwa mwanzo wake wa kuamini kwamba yeye ni mshindi.

“Nawashukuru sana SportPesa, wameniongezea mtaji mwingine hii ni faraja kwangu naamini bajaj hii itaniinua zaidi kiuchumi na kuboresha shughuli zangu za kila siku ninazofanya kujiingizia kipato, mbali na hilo nilikuwa natamani kujenga nyumba yangu ya kuishi kwa muda mrefu naona sasa jambo hili linaenda kutimia sasa,” alisema Rashid.

Aidha aliipongeza SportPesa kwa kuendelea kuwajali wateja wake na kutoa huduma bora zaidi huku akieleza hakuna jambo ambalo huwa analifurahia kutoka SportPesa kama kitendo cha mtu kubashiri halafu akashinda pesa.

“Muda huo huo baada ya mechi kumalizika, mtu anapokea hapo hapo kiasi alichoshinda, hilo ni miongoni mwa mambo ambayo mimi huyafurahia,” alisema Rashid.

Meneja Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya, aliwakumbusha watu namna ya kubashiri ambapo moja kwa moja wanaingia kwenye droo ya bajaj.

“Kwa wale ambao bado hawajajiunga na SportPesa piga *150*87# kupitia simu yako ya mkononi hapo utafanikiwa kujisajili na utaweka pesa na kuanza kucheza,” alisema Sabrina .

Malick Rashid akionyesha bajaj aliyokabidhiwa na timu ya Shinda Zaidi na SportsPesa mkoani Morogoro. Picha na mpigapicha wetu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.