MWALALA AIPA YANGA MBINU ZA UBINGWA.

Bingwa - - BONGO -

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Ben Mwalala raia wa Kenya, amewataka viongozi wa klabu hiyo, kuwathamini wachezaji wao ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Akizungumza na BINGWA juzi, Mwalala, alisema wachezaji wanapaswa kupewa stahiki zao kwa wakati ili waweze kutimiza malengo yaliyowekwa na viongozi wao, yakiwamo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Yanga uongozi unaleta shida, zamani wachezaji walikuwa wakilipwa kwa wakati na timu ilikuwa ikifanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo viongozi wahakikishe wanatimiza wajibu wao,” alisema Mwalala.

Mwalala alisema iwapo viongozi hao watatimiza wajibu wao ipasavyo itasaidia klabu yao kupata mafanikio kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mshambuliaji huyo, aliyeichezea Yanga kwa mafanikio makubwa, alisema baadhi ya wachezaji morali ya kucheza imeshuka kutokana na kushindwa kulipwa kwa wakati.

Mwalala ambaye aliwahi kuichezea Coastal Unioni ya Tanga, kwa sasa ni kocha wa timu ya Bandari ya Mombasa inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.