Ramsey: Huyu Aubameyang ni kama Thierry Henry

Bingwa - - MAKALA -

NYOTA wa Arsenal, Aaron Ramsey, amemfananisha mwenzake, PierreEmerick Aubameyang, kama staa wa zamani wa timu hiyo, Thierry Henry, kwa jinsi anavyocheza na umaliziaji.

Juzi Ramsey alikuwa amekaa benchi wakati Aubameyang akipachika mabao mawili yaliyoifanya Arsenal kuondoka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Tottenham katika mtanange wa ‘North London derby’ uliopigwa katika Uwanja wa Emirates.

Kutokana na umaliziaji wa staa huyo, kiungo Ramsey anaelezea jinsi alivyokunwa na staa mwenzake, Aubameyang aliyeyafanya matokeo kuwa sare ya 2-2 kabla ya wenzake, Alexandre Lacazette na Lucas Torreira, kuing’arisha Gunners.

"Huwezi kuamini, lakini amekuwa akifanya hivyo mara zote mazoezini," alisema Ramsey.

"Ana uwezo wa kufanya hivyo mipira ya kona lakini hata pia ni mzuri kwa pasi. Ananikumbusha umaliziaji wa Thierry Henry,” aliongeza staa huyo.

Alisema kwamba, anavyodhani ni mtu muhimu kwao kuwafungia mabao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.