Wamvamia refa njiani

Bingwa - - JUMANNE SPESHO | UNAKOSAJE? -

MASHABIKI wa Samunge FC wamemvamia na kumdunda mwamuzi, Juma Isaya aliyechezesha mchezo wa Kombe la Kuku kati yao na Kijiti, wakidai kuwa alipewa fedha na wapinzani wao kwani alikuwa akipendelea upande mmoja. Akizungumzia tukio hilo lililotokea juzi, mwamuzi huyo alisema alikuwa akielekea dukani kufanya mahitaji yake, lakini alishangaa kundi la vijana wakimvamia na kuanza kumpiga, alipowauliza walidai kuwa alishindwa kufanya maamuzi sahihi katika mechi hiyo na kuwapendelea wapinzani wao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.