JIFUNZE LINGALA NA NOAH YONGOLO

Bingwa - - KONA YA BOLINGO -

NAPENDA kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona siku ya leo, mimi si mjanja sana kuliko wengine bali ni neema yake tu kwani kuna wengi siku ya leo hawajaiona, wengine ni wagonjwa wako mahospitalini na majumbani. Bila shaka nawe kakujalia neema hii, naomba nikukaribishe tena kwenye darasa la kujifunza Lingala kama ilivyo ada.

Wiki mbili zilizopita tumekuwa tukijifunza kwa kuunda sentensi, leo tutabadili kidogo kwa kukufundisha neno moja moja ili baadaye tuundie sentesi.

Tuanze darasa letu kwa mtiririko huu kama ifuatavyo hapa chini;

Ezali / Ni, Ipo; Ekeseni / Inapishana, Inatofautiana / Tofauti; Masanga ya Mbila /Pombe ya mchikichi; Mboloko / Swala; Okomi Kwitikwiti / Umekuwa mlevi; Na lolenge mosusu / Kwa maneno mengine.

Etikee / Yatima; Mwana etikee / Mtoto yatima; Bompangi / Ufitina, Fitina; Misisa / Mishipa; Mikuwa / Mifupa; Misuni / Minofu; Komata mapapu /Kuota mbawa; Atandele / Iko siku; Bampangi / Wafitini; Mbuma eteli / Tunda limeiva.

Kolikiya / Kuhitimisha, kufika kikomo; Suka /Kikomo, Hatima; Mokumba ya bana / Msururu wa watoto; Mayi ya molimo /Maji ya uzima; Longola bobangi / Ondoa hofu; Libota kino libota / Kizazi hadi kizazi; Kosolo, Kozolo / Kunuka.

Kobatama /Kufichama ndani ya kitu.

Mwanafunzi na msomaji wangu kwa leo tumefika mwisho wa somo letu, tutaendelea na darasa hili Jumanne ijayo, alamsiki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.