Tanzania Prisons wataja kinachowamaliza

Bingwa - - HABARI - NA ZAINAB IDDY

KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohammed 'Bares', amesema kuwa msimu huu kikosi kimekosa mwenendo mzuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na mara nyingi mabeki wake kukubali kufanya makosa ya kizembe.

Katika msimamo wa ligi, hadi sasa Prisons wana pointi 10 walizozipata katika michezo 15 waliyocheza, ambapo wamepoteza mechi 7, sare 6 na kushinda mchezo mmoja pekee na hivyo kujikuta wakiwa nafasi ya 19.

Akizungumza na BINGWA, Abdallah, alisema wamekuwa na mwanzo mzuri katika michezo yao mingi, lakini mwisho wachezaji wake wameshindwa kutimiza majukumu yao.“Naumiza kichwa kuwafikiria wachezaji wangu hususan upande wa mabeki, mara nyingi katika kipindi cha kwanza wanalinda vizuri lakini kikianza tu kipindi cha pili ndipo ujinga mwingi unafanyika.

“Mfano mzuri mechi yetu iliyopita dhidi ya Yanga, tulianza vizuri lakini kipindi cha pili mabeki walianza kukosa utulivu hadi tukafungwa mabao 3-1, hii si mara ya kwanza hakika wachezaji wanachosha,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.