NJOMBE MJI KUSAJILI SABAWAPYA

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

KLABU ya Njombe Mji inatarajia kusajili wachezaji saba wapya katika dirisha dogo ili kukiboresha kikosi chake kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ali Bushiri, alisema atasajili wachezaji hao ili kuziba nafasi kwa wale walioondoka na kujiunga na klabu nyingine.

Bushiri alisema baadhi ya wachezaji wameruhusiwa kujiunga na timu nyingine hivyo wamejipanga kutumia dirisha dogo kujaza nafasi zao.

Alitaja wachezaji walioondoka ni Dany Mrwanda, Juma Jabu, Mayala Membe na Manzi Notkei.

“Kwa sasa nina wachezaji wanaofanya majaribio katika timu yangu, hivyo naendelea kuwaangalia kama wanafaa kusajiliwa,” alisema Bushiri.

Njombe Mji ilishuka daraja Ligi Kuu msimu uliopita wa 2017/18 kutokana na kufanya vibaya katika michezo yao.

Mratibu wa Usambazaji na Tigo Pesa Mkoa wa Kilimanjaro, Wolfgan Miraro (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh milioni moja, mmoja wa washindi wa Promosheni ya Jigftishe, Yussuph Miraro wa mkoani Arusha. Na Mpigapicha Wetu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.