Licha kukaliwa kooni na UEFA, Fifa kuipa mamilioni ya pauni Man City

Bingwa - - EXTRA -

ZURICH, Uswisi

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), litaipa Manchester City kitita cha pauni milioni 3.9 kutoka kwenye faida ambayo lilipata katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia kama ulivyo utaratibu wake wa kugawana na klabu.

Katika mgao huo, kwa ujumla Fifa itatoa kitita cha pauni milioni 164 ilizozipata katika fainali hizo zilizofanyika nchini Urusi kwa klabu 416 kutoka mataifa 63 kiasi ambacho ni karibia mara tatu ya kile ilichokitoa katika zile zilizofanyika nchini Brazil mwaka 2014.

Tanagazo hilo la Fifa limekuja siku moja baada ya Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya UEFA, Aleksander Ceferin, kusema kuwa bodi hiyo inajiandaa kuchukua hatua dhidi ya Man City kufuatia uvunjaji wa kanuni ya matumizi ya fedha (FFP).

Mwaka 2014 Man City ilipigwa faini ya pauni milioni 50 kwa kuvunja kanuni hiyo ya FFP na huku vile vile UEFA ikiweka mipaka ya kikosi chake na matumizi ya klabu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.