Valverde ashangaa Messi kushika nafsi ya tano Ballon d´Or

Bingwa - - EXTRA -

MADRID,Hispania

KOCHA wa Barcelona, Ernesto Valverde amesema kwamba kitendo cha straika wake, Lionel Messi kushika nafasi ya tano katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji borawa mwaka wa dunia Ballon d'Or ni jambo la kushangaza.

Messi ni mshindi mara tano wa tuzo hiyo na kwa kipindi cha miaka 10 amekuwa akiipokezana na hasimu wake, Cristiano Ronaldo,lakini juzi ikashuhudiwa ikienda kwa nyota wa Real Madrid, Luka Modric.

Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2006 kwa Messi kumaliza mbio hizo akiwa nje ya orodha ya wachezaji watatu bora na huku Ronaldo, Antoine Griezmann na Kylian Mbappe wakilaza wakiwa mbele yake.

Na wakati Valverde alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu matokeo hayo alisema kwamba kitendo cha kuona Messi akiwa nafasi ya tano ni vigumu kukifafanua.

"Siwezi kuzungumza zaidi kuhusu jambo hili kama ilikuwa sahihi ama makosakwajinsi tuzo ilivyomalizika,"alisema kocha huyo.

"Nafikiri watu waliopigwakura ndio wana jibukuhusu hilo . Kila mmoja ana maoni yake lakini kwetu sisi ni ajabu. Tunampongeza Modric kwa ushindi wake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.