Maandamano yavuruga ligi Ufaransa

Bingwa - - EXTRA -

PARIS, Ufaransa

SAFARI ya timu ya Lyon kwenda kuivaa Toulouse mwishoni mwa wiki imeahirishwa kufuatia ushauri wa kamanda wa polisi katika mkoa huo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kamanda huyo wa polisi ameshauri mechi hiyo ya Ligue 1 iahirishwe kufuatia maandamano yanayoendelea katika mji huo wa Toulouse.

Taarifa zinaeleza kwamba, watu 57 wakiwano maofisa 48 wa polisi walijeruhiwa Desemba mosi, baada ya kutokea makabiliano katika maandamano hayo yanayoelezewa kuwa ni ya ghasia.

Mbali na majeruhi, pia watu 16 walikamatwa na polisi na mpaka sasa wapo rumande baada ya maduka mawili yaliyopo katikati mwa mji kuporwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.