ALIYEKUNYWA SODA SITA NA KAHAWA AVISHWA KHANGA

Bingwa - - MAKALA -

DAH, huyu jamaa sasa atakuwa na mkosi maana siku si nyingi alitoka kuwekewa soda sita na kahawa nne akasimamiwa na kunywa mpaka zilipomalizika.

Juzi tena mwanakwetu huyu anayeitwa Dullah Mohamed, ambaye ni shabiki lialia wa Yanga na Aseno, akatamba kama mnyama (Simba) atashinda kwenye ndiki yake ya Mbabane, basi yeye avalishwe khanga.

Waswazi wa kipande kile hawana dogo. Mbugi likaanza kumenyeka na matokeo ya ndiki ndiyo kama mlivyoona na kusikia. Ikabidi mwanawane wamkamate jamaa huku wakishangilia kwa nguvu na kumvalisha alichokiomba yaani khanga!

Taarifa inatolewa na Mama Komba mmiliki wa chimbo la Takwimu Stadium lililopo kipande cha Changanyikeni.

Ebwana eeh, leo ilibidi kichafuke cha ndiki za wikiendi iliyopita kutokana na hilo pia mzee baba hakutaka kukubali mwaliko wowote wa ndiki ya juzi kati ya mnyama na Mbabane ambao walibamizwa ‘4G’, lakini kutokana na tukio la Dullah, imebidi aachane na mambo ya wikiendi na kuwawekea cha juzi, shuka nayo mwanangu.

Mwanakwetu mara hii mzee wa Kibandaumiza alitembelea kipande cha Sinza, lakini ilikuwa ni katika chimbo jingine kabisa linalosonga kwa jina la Umati Stadium.

Hapa anasimama Michael Mwinyimvua kwenye uchanjaji, lakini pia ndiye mmiliki wa chimbo hili.

Ndani yake kuna runinga mbili na huduma ya vinywaji inapatikana hapo yaani namaanisha na wale wazee wa gambe hapo mwanakwetu ni mahala pake pia, ingawa inchaji anashauri ukiwa mitungi huruhusiwi kuendelea kubishana hapo kuhusu mbugi.

Hapa mwanakwetu jero inahusika sana mlangoni siku ambayo kuna mechi za nyumbani lakini kikichafuka cha majuu, buku ndiyo mpango mzima mlangoni na hii haitahusiana na kinywaji unachokunywa.

Hapa mwanakwetu wanazama waswazi 150 ingawa siku kilipochafuka Mnyama na Mbabane nyomi lilikuwa shazi zaidi.

Pande za Sinza hasa ndani ya Kibandaumiza cha Umati,

huwaambii kitu kwa ndiki za England na inanoga zaidi kinapochafuka cha timu kubwa mwanakwetu, La Liga inashika nafasi ya tatu wakati ligi ya wahapahapa inashika nafasi ya pili kwa kutazamwa tena unaambiwa siku hizi timu zenye ligi yao zikicheza panakuwa hapatoshi mwanakwetu.

Ni hayo tu kwa leo waswazi wenzangu na mimi ngoja nipite hivi baada ya machache niliyokumegea kutoka kipande hiki cha Sinza ndani ya Kibandaumiza cha Umati Stadium, kama na wewe unaonesha mpira sehemu yoyote linaposomwa gazeti la BINGWA basi unaweza kumwalika mzee wa Kibandaumiza kwa namba hizo hapo juu na atakufikia. HAWA JAMAA KILA WAKIINGIA KIBANDANI WAPO TILALILA

Abou Sechambo, James Mgaya, Athur Mwakitosi, John Msukuma, Adam Mshamu na Shukuru Kinyozi.

Kibandani kwenu nani kila akiingia kucheki ndiki lazima apige mzinga wa jero? SMS TU

Nilipokuacha: Mbugi, Ndiki- Mechi Tilalila- Kulewa chakari Mtata- Mbishi Kuchanja- Kudai Lialia- Shabiki sana Kipande hiki- Eneo hili Kudeku- Kutazama Wanazama- Wanaingia

Hapa anasimama Michael Mwinyimvua kwenye uchanjaji, lakini pia ndiye mmiliki wa chimbo hili.

Waswazi wakifuatilia ndiki ndani ya Kibandaumiza

Dulah Mohamed akinywa soda sita na Kahawa nne, hapo ilikuwa ni siku ilipocheza Arsenal na Manchester mswazi huyu ndiye aliyevalishwa khanga kwenye mechi ya juzi baada ya kuomba afanyiwe hivyo kama Simba ikishinda.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.