HASSAN DILUNGA

Kifaa cha Aussems aliyetamani kuwa mfanyabiashara

Bingwa - - MAKALA -

HASSAN Dilunga ni kiungo ambaye amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili na mabingwa watatezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC.

Kabla ya kujiunga na Simba, Dilunga alifanikiwa kuisaidia Mtibwa Sugar kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambaye naye aliibuka mchezaji bora wa mashindano hayo.

Dilunga alirejea Simba SC baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka mitano na klabu hiyo ikijaribu kumsajili kutoka Ruvu Shooting, lakini wakazidiwa kete na mahasimu wao, Yanga SC waliokuwa wanatambia fedha za mfadhili na Mwenyekiti wao wa wakati huo, Yussuf Manji.

Baada ya misimu miwili Dilunga aliondoka Yanga kufuatia kutofautiana na Katibu wao wakati huo, Jonas Tiboroha na kurejea Ruvu Shooting katika Ligi Daraja la Kwanza hadi kuisaidia kupanda Ligi Kuu, kabla ya kuhamia JKT Ruvu (JKT Tanzania) na baadaye Mtibwa.

Je, ulishawahi kujiuliza kama si soka Dilunga angefanya kazi gani?

Akizungumza na BINGWA juzi, Dilunga, alisema kama si soka angekuwa mfayabiashara mbalimbali hapa nchini na anaamini kazi ambayo ingemnufaisha sana kuliko kazi za kuajiriwa.

“Kazi za kuajiriwa mara nyingi mshahara wake hautabiriki kwa sababu kuna muda mtapewa na kuna wakati mwingine hampewi kwa wakati, lakini ukifanya biashara haijalishi ni ipi unafanya unapata fedha kwa wakati bila kusubiri mwisho wa mwezi,” anasema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.