Nusu fainali daraja la tatu Geita kupigwa kesho

Bingwa - - HABARI ZA KITAA - NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

MICHEZO ya nusu fainali ya Ligi Daraja la Tatu ngazi ya Mkoa wa Geita, inatarajiwa kupigwa kesho baada ya timu zitakazochuana katika hatua hiyo kupatikana.

Timu zilizotinga nusu fainali ni Young Boys ya Nyang'hwale, Katoro Boys, Nyankumbu FC ya Geita na Masumbwe Warriors.

Michezo ya nusu fainali imepangwa kuchezwa kesho na kushokutwa katika Uwanja wa CCM Katoro, Geita, wakati fainali ikitarajiwa kupigwa Desemba 11, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Mkoa wa Geita (Gerefa), Pius Kimisha, nusu fainali ya kwanza itazikutanisha timu za Young Boys FC na Nyankumbu FC kesho, wakati Katoro Boys ikitarajiwa kumenyana na Masumbwe Warriors keshokutwa.

Aidha, Kimisha alisema ligi hiyo ilichezwa kwa ushindani mkubwa ambapo timu zikijitahidi kufuata kanuni, huku akisisitiza kwamba maandalizi ya michezo ya nusu fainali yanaendelea vizuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.