Sikia alichosema Ada, mwanamke wa kwanza kushinda Ballon d'Or

Bingwa - - HADITHI - LONDON, England

MABAO 300 akiwa ndiyo Martial amuweka kwanza na umri wa miaka 23, ingeweza njiapanda kuwa ni rekodi Mourinho maridhawa kwa straika wa timu ya wanawake ya Olympique Lyon, Ada Hegerberg, lakini hilo limeonekana halitoshi.

Mwanadada huyo raia wa Norway, usiku wa Jumatatu ya wiki hii alitajwa kuwa mshindi wa Ballon d’Or ya kwanza ya wanawake iliyoanzishwa mwaka huu, akiungana na mshindi wa ile ya wanaume, Luka Modric.

Baada ya kunyakua tuzo hiyo, Hegerberg, alitoa ujumbe mzito kwa wanasoka wa kike wanaochipukia duniani kote.

“Hii ni hatua kubwa katika soka la wanawake,” alisema Hegerberg katika hafla za utoaji wa tuzo hiyo zilizofanyika jijini Paris, Ufaransa.

“Niwashukuru France Football (jarida la soka la Ufaransa lililoanzisha Ballon d’Or), kwa kutupa fursa ya kushinda tuzo hii. Ni muhimu sana kwetu na kwa pamoja tutafanya makubwa.

“Niwaachie neno la kuwapa nguvu wanasoka wa kike wanaoibukia duniani kote. Tafadhali, mjiamini kuwa mnaweza,” aliongeza.

Lakini mara baada ya kutoa kauli hiyo, Hegerberg, alikutana na tukio la udhalilishaji kutoka kwa DJ maarufu aliyekuwa akipiga miziki katika hafla hiyo, Martin Solveig.

DJ huyo alimuuliza nyota huyo kama anaweza kucheza mtindo maarufu wa ‘Twerk’ mbele ya umati wa wanasoka wakubwa duniani na wageni waalikwa, lakini mshindi huyo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya alikataa na kuondoka jukwaani.

Mtindo huo wa kucheza ‘ku-twerk’ ulipata umaarufu mkubwa baada ya mwanamuziki, Miley Cyrus, kuonekana akiutumia katika miziki yake.

Baada ya tukio hilo, Hegerberg, alisema kuwa DJ huyo alimfuata na kumwomba msamaha kwa kilichotokea.

“Alinifuata na alionekana kuwa na huzuni kwani hakutegemea kama ingekuwa vile. Sikuwaza kama alinidhalilisha kijinsia kwa wakati ule kwa sababu furaha yangu ilikuwa kwenye Ballon d'Or,” alisema nyota huyo.

Hegerberg aliweka rekodi ya kipekee katika msimu uliopita wa michuano ya Ulaya, ambapo alifunga mabao 15 hadi timu yake ya Lyon iliponyakua ubingwa, jumla akiwa na mabao 41 katika mechi 41 za michuano hiyo.

Mpachika mabao huyo amekuwa bora zaidi tangu atue Lyon mwaka 2014 akitokea Turbine Potsdam ya Ujerumani, akikumbukwa kwa rekodi yake ya kucheka na nyavu mara 26 katika mechi 22 za kwanza tu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.