RONALDOE

MESSI KUJIFARIJ BERNABEU

Bingwa - - HADITHI - MADRID, Hispania

BAADA ya wote kukosa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya kwanza mwaka huu, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, wanatarajiwa kuhudhuria fainali ya Copa Libertadores ambayo imehamishiwa Barani Ulaya.

Fainali hiyo ya pili ya michuano hiyo kati ya Boca Juniors na River Plate, inatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu, unaomilikiwa na klabu ya zamani ya Ronaldo, Real Madrid.

Ikumbukwe kuwa mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa wiki mbili zilizopita katika dimba la Monumental, lakini ilishindikana kutokana na fujo za mashabiki wa timu hizo za Argentina zenye upinzani mkali zaidi duniani.

Taarifa zinadai kwamba Messi ameliomba shirikisho la soka nchini kwao, AFA kumfanyia mpango wa tiketi za kuingia kwenye fainali hiyo, huku Ronaldo yeye akidaiwa kuitegemea zaidi Real Madrid katika suala la tiketi.

Tiketi hizo zinadaiwa kwamba zitawahusu nyota hao na familia zao, wake na watoto.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.