MBAPPE ATABIRIWA KUMFIKIA DE LIMA

Bingwa - - MBELE - PARIS,Ufaransa

NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Youri Djorkaeff amesema kwamba straika wa wa binara wa soka katika michuano ya Ligue 1, Paris Saint Germains, Kylian Mbappe kwa sasa yupo sawa, Thierry Henry lakini akasema kuwa atamfikia Ronaldo de Lima katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Mbappe mwenye umri wa miaka 19 tayari kwa sasa anadsemekana kuwa mmoja kati ya wachezaji bora duniani na juzi alishika nafasi ya nne katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bowa wa mwaka ya dunia, Ballon d'Or baada ya kuwa na mwaka mzuri akiwa na timu yake ya PSG na ya Taifa ya Ufaransa.

Msimu huu,straika huyo kinda ameisaidia Ufaransa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia na huku tayari ameshafunga mabao 14 katika mechi 15 alizokwisha ichezea PSG.

Kufuatia mafanikio hayo, Djorkaeff, ambaye aliisaidia Ufaransa kutwaa ubingwawaKombe la Dunia mwaka 1998 anasema kwamba katika mawazo yake anafikiri Mbappe kwa sasa ni kama Henry,lakini hivi karibuni atakuwakama kinara wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Ronaldo.

"Ana bahati ya kucheza na mastarika mahiri. Na ninavyofikiri Mbappe ni mzuri kama Thierry Henry, kwa sababu ana kasi kama yake," mkongwe huyo aliuambia mtandao wa Omnisport.

"Ronaldo alikuwa akiunasa mpira akageuka, akapiga chenga kwa kasi ya na umahiri wa hali ya juu. Lakini Mbappe anapenda kuambaa na mpira kama alivyokuwa akifanya Thierry Henry,”aliongeza nyota huyo wa zamani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.