Wawakilishi Temeke kujulikana Des 12

Bingwa - - HABARI - NA WINFRIDA MTOI

WAWAKILISHI wa Temeke katika Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, wanatarajiwa kupatikana Desemba 12, mwaka huu.

Timu tano zitakazoshika nafasi za juu katika Ligi Daraja la Tatu Wilaya ya Temeke zitaungana na nyingine za wilaya ya Ilala, Ubungo, Kinondoni na Kigamboni kushiriki Ligi Daraja Pili Mkoa wa Dar es Salaam itakayoanza hivi karibuni.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu wa Mashindano wa Chama cha Soka Wilaya ya Temeke (Tefa), Mbaraka Mohammed, alisema ligi yao imefikia katika hatua nzuri na timu zinaonyesha ushindani mkubwa wa soka.

“Hatua tuliyofikia ni lala salama, tunatafuta timu tano zitakazotuwakilisha katika Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Mohammed.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.