Riadha ya wazi kufanyika Desemba 14

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

MICHUANO ya wazi ya riadha inatarajia kufanyika Desemba 14, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday, alisema wameamua kufanya michuano ya wazi badala ya Taifa ili kupunguza gharama ya uendeshaji.

Gidabuday alisema wanariadha wote wanatakiwa kujitokeza kushiriki michuano hiyo ili kulinda viwango vyao.

Alisema wanariadha watashiriki katika mbio za mita 100, 10,000, miruko na mitupu na washindi watazawadiwa fedha taslimu na medali.

Washindi wa kwanza watazawadiwa Sh 200,000, washindi wa pili Sh 150,000 na washindi wa tatu Sh 100,000.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.