Bosi Mawenzi Market abwaga manyanga

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

KATIBU Mkuu wa Klabu ya Mawenzi Market, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara ya mkoani Morogoro, Zemu Mbilu, ameachia ngazi kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kiserikali.

Akizungumza na BINGWA jana, Mbilu, alisema amechukua uamuzi huo ili aweze kutimiza kwa ufasaha majukumu yake.

Mbilu alisema hawezi kuendelea na majukumu mawili, hivyo ataendelea kuwa ni mwanachama wa kawaida wa Mawenzi Market.

“Nimejiuzulu kutokana na kuzidiwa majukumu, lakini nitaendelea kutoa sapoti kwa Mawenzi Market nikihitajika,” alisema Mbilu.

Alisema ataendelea kushirikiana na viongozi wa klabu hiyo ili kuiwezesha timu yao kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.