JANJARO KUMFANYIA MAKUBWA ZAIDI MAMA YAKE

Bingwa - - EXTRA - NA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kumjengea nyumba ya kisasa mama yake mzazi maeneo ya Sombetini, Arusha rapa Abdul Chende ‘Janjaro’, amepanga kuendelea kumfanyia makubwa mzazi wake huyo ili afurahie matunda yake.

Janjaro ambaye juzi jijini humo alifanya dua maalumu ya kumwombea marehemu baba yake, ameliambia Papaso la Burudani kuwa fedha alizotumia kujenga nyumba hiyo ya kisasa imetokana na muziki.

“Mzazi akifurahi ndiyo baraka zenyewe zinakuja, nyumba ina jumla ya vyumba vitatu vizuri na ya kisasa, hiki ni kitu kidogo bado naendelea kufikiria mengine makubwa zaidi ya kumfanyia mama yangu,” alisema Janjaro.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.