Mourinho akana kutengwa na mastaa wake

Bingwa - - EXTRA - LONDON,England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amekanusha madai ya kwamba haungwi mkono na wachezaji wake, akisema kwamba kiwango kinachooneshwa na mastaa wake waaminifu ndicho kinachodhihirisha jinsi wanavyompenda bosi wao.

Kwa mara nyingine hali ya shinikizo imezidi kupanda tena kwa Mourinho baada ya timu yake kukosa ushindi katika michezo mitatu ya Ligi Kuu England na huku ikishika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi.

Usiku wa kuamkia jana vinara haoa walikuwa wakiwakaribisha Arsenal inayoshika nafasi ya nne na kama watakuwa wamefungwa itashuhudiwa wakiwa nyuma kwa pointi 11 dhidi vijana haoa wa kocha Unai Emery.

Hata hivyo akijibu swali alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na wachezaji, Mourinho alisema kwamba wana kazi ya kufanya.

"Kama utakuwa unafikiri wachezaji wanacheza kwa kile walichoambiwa wanakuwawapo nyuma ya kocha na jinsi unavyoweza kuwaita wachezaji ama kwa suala kama hili unaweza kuwaita waaminifu,"Mreno huyo aliviambia vyombo vya habari vya Uingereza.

"Kucheza soka kunalipa na kunalipa zaidi unapokuwa mchezaji wakulipwa inakubidi ufanye mazoezi ya kutosha kila siku, ucheze kiasi cha kutosha na ili uweze kuyateka mamlioni ya mashabiki kulingana jinsi kazi hii ilivyo ni lazima uiheshimu na uongozi wa klabu,”alisema kocha huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.