Klopp aahidi kutorudia alichokifanya Anfield

Bingwa - - HADITHI - MERSEYSIDE, England

KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amesema kwamba hatarudia ushangiliaji uliovuka mipaka kama aliouonesha wikiendi iliyopita baada ya straika wake, Divock Origi, kufunga bao la ushindi dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Everton.

KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema kwamba hatarudia ushangiliaji uliovuka mipaka kama aliouonesha wikiendi iliyopita baada ya straika wake, Divock Origi kufunga bao la ushindi dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Everton.

Klopp alionekana kuzidiwa na hisia kali za furaha kwa kushangilia hadi ndani ya uwanja kabla ya filimbi ya mwisho kupigwa, baada ya bao hilo lililofungwa katika dakika za lala salama wakati mchezo huo ukionekana kumalizika kwa timu hizo kutofungana. Kutokana na kitendo hicho, Klopp alilimwa faini ya pauni 8,000 na chama cha soka nchini Engand, FA, lakini alisisitiza kwamba hatafanya kosa hilo tena. “Sikuwa na nia ya kuwavunjia heshima wapinzani. Naomba radhi na sitarudia tena kuvunja sheria. Adhabu ya kulipa faini ni onyo kubwa zaidi kwangu na kwa rekodi tu, imepita miaka 14 tangu hili litokee (mara ya kwanza akiwa Mainz mwaka 2004,” alisema

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.