Ngoma afurahia kucheza na Chirwa Azam

Bingwa - - HABARI/TANGAZO - NA TIMA SIKILO

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Donald Ngoma, ameelezea kufurahishwa na ushirikiano kati yake na Mzambia Obrey Chirwa, ambao unazaa matunda katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Ngoma na Chirwa walisajiliwa hivi karibuni na Azam, lakini ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora katika michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.

Ngoma aliliambia BINGWA kuwa, malengo yake ni kufanya vizuri katika mashindano yote ili aendelee kuwa changuo la kocha, Hans van der Pluijm. Alisisitiza kwamba, ushirikiano wake na Chirwa ni mzuri na anaufurahia kwa sababu hata kocha anayewapanga pamoja anaamini umoja huo unaweza kuwa na mafanikio kikosini.

Aidha, Ngoma aliongeza kuwa anafurahia kufundishwa na Pluijm kwani ni kocha ambaye amekuwa akimthamini na kumlea kama mtoto wake.

Ngoma na Chirwa wote waliwahi kuichezea Yanga kipindi ikifundishwa na Pluijm, lakini kila mmoja akaondoka kwa wakati wake na baadaye kuja kukutana tena Azam.

Chirwa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.