Kocha Ruvu Shooting aivutia kasi KMC

Bingwa - - HABARI/TANGAZO - NA EDITHA NORASCO (FJS)

KOCHA mkuu wa timu ya Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji, amesema anatambua uwezo wa kikosi cha KMC hivyo anaamini mbinu alizowapa wachezaji wake zitasaidia kupata matokeo bora.

Ruvu Shooting wanatarajia kuvaana na KMC leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kutoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC.

Akizungumza na BINGWA jana, Haji alisema anaamini mbinu na maelekezo aliyotoa kwa wachezaji vitasaidia kuzaa matunda na kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo.

“Wachezaji wamejifua vizuri na kikosi kipo imara tayari kuwakabili wapinzani wetu kesho (leo), tutapambana kusaka pointi tatu muhimu.

“Tunacheza uwanja wa ugenini hivyo tunawaomba mashabiki wetu watuombee na kuzidi kutupa sapoti na hamasa ya ushindi,” alisema Haji.

Ruvu Shooting inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuvuna pointi 23 katika michezo 20 iliyochezwa, wakipata sare tano, kufungwa tisa na kushinda sita.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.