Mwakasonda ni mgombea anayekuja na mtazamo mpya Yanga SC

Bingwa - - MAONI MTAZAMO KATUNI - NA ONESMO KAPINGA

JINA la Benjamin Mwakasonda si geni kwa wanafamilia ya soka hapa nchini, kutokana na mchango wake katika maendeleo ya soka.

Pamoja na shughuli nyingine anazofanya katika maendeleo ya nchi hii, lakini amekuwa ni mtu muhimu hasa kutokana na jitihada zake za kuibua vipaji chipukizi na kusimamia utawala bora katika soka.

Mwakasonda ni miongoni mwa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi ya uongozi katika uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga, uliopangwa kufanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kiufupi, Mwakasonda ni mwanamichezo, hususan soka, lakini ni mwanachama wa Yanga anayewania nafasi ya Kamati ya Utendaji, akiwa na mtazamo tofauti wa kimawazo katika kuiongoza klabu hiyo.

Lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha anaitoa Yanga hapo ilipo na kuifikisha katika hatua nyingine ya kimaendaleo ndani na nje ya Tanzania.

Moja ya malengo ya mgombea huyo ni kuhakikisha anashirikiana na viongozi wengine watakaochaguliwa Jumapili kusimamia Katiba ya Klabu hiyo ili kuleta maendeleo ya soka.

Kwa kuwa Katiba ya Yanga ni mwongozo katika kuongoza klabu, atahakikisha anashauri kuhakikisha mali zake hazitumiki hovyo kwa maslahi ya watu wachache.

Mgombea huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria, atahakikisha analinda Katiba ya Yanga na utajiri wake ili utumike ipasavyo kwa maendeleo yake.

Yanga ina utajiri mkubwa wa rasilimali watu na vitega uchumi vingine, hivyo akipata ridhaa ya wanachama kuwa miongoni mwa viongozi watakaochaguliwa Jumapili atahakikisha klabu hiyo

Pia Yanga ni timu kubwa, ina uwezo mzuri, hivyo atahakikisha anashirikiana na viongozi wenzake watakaochaguliwa kusimamia mauzo ya jezi za wachezaji wa klabu hiyo, ili iweze kujiingizia kipato.

inanufaika na utajiri wake.

Jambo lingine wanalokusudia kulifanya akipata ridhaa ya kuchaguliwa ni kuhakikisha klabu hiyo inakuwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka miaka 20, 17, 16 na 14, ili baadaye kupata wachezaji bora ambao watakuwa tegemeo kwa klabu hiyo.

Pia Yanga ni timu kubwa, ina uwezo mzuri, hivyo atahakikisha anashirikiana na viongozi wenzake watakaochaguliwa kusimamia mauzo ya jezi za wachezaji wa klabu hiyo, ili iweze kujiingizia kipato.

Kutokana na ukongwe wa klabu hiyo, Mwakasonda anaweza kusimamia maendeleo ya soka ya vijana ambao ni uti wa mgongo wa timu na nchi yoyote ambayo imepiga hatua katika soka.

Kwa kiasi kikubwa ana uzoefu mkubwa wa kusimamia soka ya vijana, lakini pia masuala ya utawala bora wa mpira wa miguu ambaye kwa sasa mgombea huyo ni mwenyekiti mwanzilishi wa Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (Ufa).

Uzoefu katika uongozi wa soka ndio uliomsukuma kuwania nafasi ya kamati ya utendaji, akiamini atatumia taaluma yake kuipa mafanikio makubwa klabu hiyo, hasa katika kipindi hiki ambacho Yanga inahitaji mabadiliko ya kweli ili kwenda sambamba na mahitaji ya mpira wa miguu.

Mtazamo wa Mwakasonda ni kutaka kuifanya Yanga kuwa ya kimataifa zaidi, lakini ikianzia kupata maendeleo katika michuano ya ndani, ikiwamo Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Hilo linawezekana, kwani kinachohitajika ni mipango ya pamoja ya wanachama, viongozi na wadau wengine wa klabu hiyo kuhakikisha kila jambo linalopangwa linapata mafanikio.

Mwakasonda anaomba wanachama kutofanya makosa katika uchaguzi huu, hivyo ni jukumu lao kupima sera za kila mgombea kabla ya kufanya uamuzi wa kupiga kura.

Mwakasonda

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.