WACHEZAJI BIASHARA WAWEKA KIKAO KIZITO

Bingwa - - HABARI - NA SHOMARI BINDA, MUSOMA

WACHEZAJI wa Biashara United wamefanya kikao kizito cha kujenga mkakati wa kushinda mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, utakaochezwa kesho Uwanja wa Karume mjini Musoma.

Akizungumza na BINGWA juzi baada ya kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa timu hiyo, nahodha wa Biashara United, Kauswa Bernard, alisema wameweka mkakati madhubuti kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

Bernard alisema wachezaji wameamua kukutana na moja ya mambo waliyokubaliana ni kucheza kwa kujituma na kuwa kitu kimoja kuhakikisha matokeo ya ushindi yanapatikana.

Alisema katika kikao hicho walikubaliana kufuata maelekezo yote ya uongozi na benchi la ufundi ili kutimiza malengo yao.

Nahodha huyo alisema iwapo wachezaji wakizingatia maelekezo kutoka benchi la ufundi na uongozi wa timu hiyo ushindi utapatikana.

"Tumekutana kukubaliana kujituma na kufuata maelekezo ili kuweza kufikia malengo," alisema Kauswa.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa timu hiyo, wamemmwagia sifa kocha wao mpya, Amri Said, kutokana na uwezo wa kufundisha soka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.