Kisaka kocha mpya Pamba

Bingwa - - HABARI - NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

KOCHA Ally Kisaka, amepewa jukumu la kuifundisha timu ya Pamba inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL).

Kisaka ameingia makubaliano ya kuifundisha timu ya Pamba hadi mwisho wa msimu wa ligi hiyo, akichukua nafasi ya kocha aliyemtangulia, Juma Sumbu, anayesumbuliwa na maradhi.

Sumbu aliajiriwa na Pamba Septemba 5, mwaka jana kabla ya kuanza kwa ligi hiyo akitokea timu ya Chuoni ya Zanzibar, lakini ameshindwa kuendelea na majukumu yake kutokana na maradhi ya moyo na kupooza mwili.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa klabu hiyo, Johnson James, Kisaka mwenye leseni C ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), atakuwa kocha wa muda wa timu hiyo.

"Klabu ya Pamba imeingia makubaliano na Kisaka kutokana na aliyekuwa kocha wetu kuugua ghafla na kushindwa kuendelea na majukumu yake,” alisema James.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.