Kocha Marsh Girls aanika mapungufu

Bingwa - - HABARI - NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

KOCHA wa timu ya Marsh Girls, inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (SWPL), George Aaron, ametaja sababu za kutofanya vizuri katika ligi hiyo.

Akizungumza na BINGWA juzi, Aaron alisema wachezaji wake wanakosa umakini na uzoefu katika mikikimikiki ya ligi hiyo.

Alisema kutokana na sababu hiyo, timu yake imeshindwa kupata ushindi katika michezo mitatu mfululizo.

Kocha huyo alisema hadi sasa wamepata sare mbili kutoka kwa Mapinduzi Queens na Evergreen Queens na kuchapwa bao 1-0 na Yanga Princess.

Aaron alisema kutokana na mapungufu kwenye kikosi chake, anahitaji kusajili wachezaji wazoefu sita katika dirisha dogo, wakiwamo walinzi wawili, viungo wawili na washambuliaji wawili.

"Naangushwa na umakini wa wachezaji, tunashindwa kupata matokeo kwa sababu wanatengeneza nafasi zaidi ya sita lakini hawazitumii.

"Tutaangalia dirisha dogo tuone tunafanya nini kuboresha kikosi, hasa tunahitaji wachezaji wazoefu, mashabiki waendelee kuvuta subira na uvumilivu," alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.