Mourinho, Man Utd wabwagana rasmi

Bingwa - - SPORTS -

LONDON, England

TIMU ya Manchester United na aliyekuwa kocha wao, Jose Mourinho, wamebwagana rasmi, baada ya kumlipa Mreno huyo kikita cha pauni milioni 15, kama fidia kwa kumfukuza.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55, alifukuzwa Desemba 18, mwaka jana, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.

Kufuatia hali hiyo, baada ya kulipwa kitita hicho kwa kuondoshwa kwenye klabu hiyo ya Old Trafford, ina maana kwamba sasa yupo huru kurejea katika majukumu ya kufundisha soka.

Chanzo cha habari kilichopo karibu na Mourinho, kilieleza usiku wa kuamkia jana kwamba kwa sasa hakuna tatizo kwenye mkataba kati ya Mourinho na Manchester United kwani kila kitu kimeshatatuliwa.

“Kwa sasa hakuna tatizo katika mkataba wa Jose na Man United kwani kila kitu kimshatatuliwa, hivyo anaweza kuanza kazi na timu nyingine, lakini haina haraka. Kwa sasa anahitaji kupumzika na angefurahi kusubiri hadi mwishoni mwa msimu kama atahitaji kufanya hivyo,” kilieleza chanzo hicho.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.