TANO KALI

Bingwa - - SPORTS -

KISA cha filamu hii iliyotoka Juni 26, 1988, kinamhusu Prince Akeem (Eddie Murphy). Ni mtoto wa mfalme wa nchi za kitajiri barani Afrika na hakuwa na shida ya kitu chochote, isipokuwa mke ambaye atampenda yeye kama yeye si kwa cheo chake. Kuepuka kuoa kwa kupangiwa, Akeem alisafiri hadi Marekani akiwa na mpambe wake, Semmi (Arsenio Hall), kumsaka ‘queen’ wake. Alijifanya mwanafunzi wa kigeni na kufanya kazi kwenye mgahawa, akampenda Lisa (Shari Headley). Kazi kubwa ilikuwa ni kumwambia ukweli msichana huyo kuwa yeye nani na kumshawishi baba yake ambaye ni mfalme (James Earl Jones). Filamu hii iliyoongozwa na John Landis imegharimu Dola za Kimarekani milioni 28 (shilingi bilioni 64).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.