Wandengereko hutumia ngoma ya spoti kuvuna

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

KABILA la Wandengereko kutoka Rufiji mkoani Pwani, ni moja ya makabila makubwa na yenye ngoma nyingi za asili.

Moja ya ngoma zao ni spoti, ambayo huchezwa kipindi cha mavuno, kutolewa kwa mwali au matukio ya kishujaa likiwa limetokea.

Spoti huchezwa kwa staili ya kupishana, ambapo wachezaji wanazunguka duara huku mdundo ukipigwa.

Wakati wengine wanaendelea kuzunguka na mdundo ukiendelea, mmoja mmoja huingia katikati na kuonyesha uwezo wake wa kucheza na watu hao hupishana kila mdundo unapobadilika na kuingia mwingine.

Wapigaji wanakuwa na ngoma mbili ambazo hazijachimbiwa chini na ngoma hizo mbili ndio hubadilisha mdundo na kumwita mtu aingie kucheza.

Wakati ngoma hiyo inapigwa kunakuwa na pombe ya mnazi na mtama, lakini hawapiki chakula kwa kuwa huwa haikeshi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.