Mtanzania amshinda Mkenya pointi 12-2

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

MCHEZAJI wa tenisi wa Tanzania, Esther Nakulege, ameibuka mshindi baada ya kumchapa Byes Trakoze wa Kenya kwa pointi 12-2 katika mchezo wa fainali wa mzunguko wa kwanza wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati inayoendelea kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. Katika mzunguko wa kwanza, Esther alishinda kwa seti 6-1 kabla ya kupata ushindi wa seti 6-1 mzunguko wa pili.

Nicolas Mella alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi 13-9 dhidi ya James Moses ambao wote ni Watanzania, alishinda seti 6-4, 7-5.

Mchezo mwingine, mchezaji Kanuti Omar wa Tanzania, alipoteza mchezo wake, baada ya kufungwa kwa pointi 12-6 dhidi ya Demick Ominde wa Kenya, aliyeshinda seti 6-1, 6-2.

Angel Outoy wa Kenya aliibuka na ushindi wa pointi 13-7 dhidi ya Alicia Owig wa Kenya, aliyeshinda seti 6-1, 6-3.

Kwa upande wake, Ismail Rashid wa Tanzania, alishindwa kutamba, baada ya kufungwa kwa pointi 13-8 dhidi ya Ndayishimiye Abubakar wa Burundi, ambaye alishinda 7-5, 6-3.

Katika mchezo mwingine, Beatrice Kimaro, aliibuka na ushindi wa pointi 12-6 dhidi ya Victoria Ndessa, ambaye alishinda seti 6-2, 6-4 wakati Adill Msale akifungwa kwa pointi 12-2 na Mateo Lavgne wa Shelisheli kwa seti 6-0, 6-2.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.