Mgunda aita chipukizi kikapu JMK Park

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

KOCHA wa mpira wa kikapu, Bahati Mgunda, amewataka wachezaji kujitokeza katika majaribio ya kucheza mchezo huo yatakayofanyika mwezi huu, viwanja vya JMK Park, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Mgunda, alisema majaribio hayo yatafanyika kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 16.

Mgunda alisema wachezaji watakaofanya vizuri watapata nafasi ya kushiriki Ligi ya Jr NBA itakayoanza Machi 8 hadi Novemba 9, mwaka huu.

“Tunahitaji kupata wachezaji watakaounda timu zisizopungua 30 kwa ajili ya kushiriki Jr NBA, hivyo kuanzia Januari mwishoni tutakuwa na mashindano ya majaribio.

“Lengo ni kuchagua wachezaji ambao watajiunga na timu zitakazofanya vizuri, tunaomba wajitokeze kwa wingi uwanjani,” alisema Mgunda.

Mgunda alisema kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji 15 walio chini ya umri wa miaka 14 waliozaliwa kuanzia mwaka 2005 hadi 2006.

Alisema timu itakayoundwa chini ya umri wa miaka 16, wachezaji wanaohitajika ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 2003 hadi 2004.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.