Uwepo wa mchezaji Coastal Union Zenji wafafanuliwa

Bingwa - - MISIMAMO RATIBA -

MENEJA wa timu ya Malindi, Kao Hojofat, ametolea ufafanuzi kuhusu mchezaji wa Coastal Union, Adeyun Salehe, ambaye anakipiga na timu hiyo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar.

Hojofat alisema mchezaji huyo aliyepewa ruhusa maalumu na timu yake ya Coastal Union kurudi kwao Zanzibar kufunga ndoa, alijumuika na kikosi cha Malindi kwa ajili ya kujipa mazoezi.

Meneja huyo ameliambia BINGWA kwamba, Adeyun bado ana mkataba na Coastal Union ya Tanga, lakini anacheza Mapinduzi Cup kama sehemu ya kujipa mazoezi baada ya kupewa ruhusa maalumu na uongozi wa timu yake.

Hojofat hawana mpango wa kumsajili Adeyun, ila yupo ndani ya kikosi chao kushiriki Kombe la Mapinduzi ambayo ni sehemu ya bonanza kujiweka fiti kabla ya kurudi kuitumikia timu yake ya Coastal Union.

Alisema hawajapokea barua wala taarifa yoyote kutoka uongozi wa Coastal Union ukiwalalamikia kumtumia mchezaji wao katika michuano hiyo ya Mapinduzi, ambayo Malindi wameingia hatua ya nusu fainali.

Hojofat alisema hata wakitoa malalamiko, nao (Coastal Union) wanatambua wamemsajili mchezaji wao, James Nyakarungu bila kupokea barua ya uhamisho na hadi sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halijatoa majibu, licha ya kupokea malalamiko yao.

Adeyum naye aliliambia BINGWA muda wake wa kurudi Coastal Union waliompa ruhusa maalumu haujakamilika na anatumia michuano hiyo kujiweka sawa sawa kabla ya kurudi Tanga.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.